Kiromania - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Kiromania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maeneo penye wasemaji wa Kiromania

Kiromania (Kiromania: român tamka "romin") ni kati ya lugha za Kirumi na lugha rasmi ya Romania na Moldova.

Asili ya Kilatini

[hariri | hariri chanzo]

Asili yake ni Kilatini ya Roma ya Kale kwa sababu sehemu kubwa ya Romania ya leo ilikuwa jimbo la Dakia katika Dola la Roma. Leo hii takriban theluthi mbili za msamiati una asili ya Kilatini, asilimia 20 ni za asili ya Kislavoni na mengine kutuoka lugha mbalimbali za jirani kama Kigiriki au Kituruki.

Wasemaji

[hariri | hariri chanzo]

Katika Romania penye wakazi milioni 22 zaidi ya milioni 19 hutumia Kiromania kama lugha ya mama. Nchini Moldova penye wakazi 4.5 karibu milioni 4 husema Kiromania inayoitwa huko "Kimoldova" lakini ni lugha ileile. Kuna pia waesamji katika nchi jirani hasa Serbia, Ukraine, Urusi (Siberia), Bulgaria na Hungaria. Waromania waliohamia huendelea kutumia lugha huko Marekani, Kanada, Australia, Israel au Uturuki. Baada ya mwisho wa ukomnisti waromania wengi wametafuta kazi na kukaa Hispania na Italia.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kiromania kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.