Kimandarini - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Kimandarini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kimandarimi
汉语 / 漢語
普通话 / 普通話
Lugha
Asili Uchina, Taiwan, Singapore, na jamii za Kichina ulimwenguni kote
Wasemaji

L1 : 929 milioni
L2: 1.2 bilioni

Jumla: 1.2 bilioni
Familia za lugha Kichina
Kisino-Tibetani
Aina za Awali Kichina cha Kale
Kichina cha Kati
Mfumo wa kuandika Herufi za Kichina
Pinyin
Zhuyin
Kilatini
Lugha Rasmi
Lugha rasmi kwa Uchina, Taiwan, Singapore, Umoja wa Mataifa (miongoni mwa lugha rasmi)
Nambari za Msimbo
ISO 639-1 zh
ISO 639-2 chi / zho
Glottolog mand1415

     Kimandarini ndio lugha kuu      Kimandarini ndio lugha ya kitaifa      Nchi zenye wazungumzaji zaidi ya 1,000,000      Nchi zenye wazungumzaji zaidi ya 500,000      Nchi zenye wazungumzaji zaidi ya 100,000]]

Kichina ni lugha za Wachina nchini China na kote duniani wanapoishi. Ni tawi kubwa la kundi la lugha za Kichina-Kitibet.

Kiwango cha asili cha Kimandarini nchini Uchina

Kimandarini ni lugha ya Kisino-Tibeti nchini Uchina inayozungumzwa na Wachina. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kimandarini nchini Uchina imehesabiwa kuwa watu milioni 840. Pia kuna wasemaji katika nchi zifuatazo: 24,320,000 nchini Taiwan (1993), 10,600 nchini Brunei (2006), 60,900 ndani ya Hong Kong (2006), 460,000 nchini Indonesia (1982), wengi nchini Malaysia ambapo ni lugha ya taifa (lakini bila idadi rasmi ya wasemaji), 35,000 nchini Mongolia (1993), 500,000 nchini Myanmar (1994), 500 nchini Ufilipino (1990), 1,210,000 nchini Singapuri (2010), na 5,880 nchini Uthai (1984). Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kimandarini iko katika kundi la Kichina.

Sauti na toni

[hariri | hariri chanzo]

Tabia ya pekee ya lugha za Kichina ni tofauti kubwa kati ya toni za sauti. Silabi "ma" inaweza kuwa na maana 4 tofauti kabisa kufuatana na matamshi tofauti ya toni.

Toni ya 1 Toni ya 2 Toni ya 3 Toni ya 4
toni ileile ya juu toni yapanda juu toni yashuka
na kupanda juu
toni ya
kushuka vikali
mā=mama má=bangi mǎ=farasi mà=kutukana

Kimandarini ni lugha rasmi katika Jamhuri ya Watu wa China, Jamhuri ya China (Taiwan) na Singapuri. Husemwa pia na raia Wachina katika Indonesia na Malaysia.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kimandarini kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.