Jack Wilshere - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Jack Wilshere

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jack Wilshere
Jack Wilshere
Youth career
2001–2008Arsenal
Senior career*
MiakaTimuApps(Gls)
2008–Arsenal2(0)
Timu ya Taifa ya Kandanda
2006–2007England U163(0)
2007–2009England U178(2)
2009–England U191(0)
2009–England U214(0)
* Senior club appearances and goals counted for the domestic league only and correct as of 18:21, 13 Desemba 2009 (UTC).

† Appearances (Goals).

‡ National team caps and goals correct as of 18:11, 8 Septemba 2009 (UTC)

Jack Andrew Wilshere (amezaliwa 1 Januari, 1992 katika sehemu ya Stevenage, Hertfordshire) ni mwanakandanda wa Uingereza anayechezea klabu ya Arsenal ya ligi kuu ya Uingereza. Kwa kawaida yeye hucheza kama kiungo wa kati anayeshambulia na hutumia mguu wa kushoto sanasana.

Wasifu wa Klabu

[hariri | hariri chanzo]

Wilshere alijiunga na Arsenal Academy mnamo Oktoba 2001 akiwa na umri wa miaka tisa, baada ya kuwa mwanafunzi katika shule ya kandanda ya Luton Town kwa miezi miwili. Alipanda safu ya Arsenal, na alipokuwa na umri wa miaka 15 alitajwa kama nahodha wa timu ya vijana ya wasiozidi umri wa miaka 16 ya Arsenal; pia aliichezea timu ya vijana wasiozidi umri wa miaka 18. Katika majira ya jua ya mwaka wa 2007 Wilshere alishiriki katika Kombe la vijana la Mabingwa na aliporejea nchini Uingereza, kocha wa Arsenal Academy, Steve Bould alimwanzisha katika mechi ya timu ya vijana wasiozidi umri wa miaka 18 dhidi ya timu ya vijana wasiozidi umri wa miaka 18 ya Chelsea. Alifunga bao lake la kwanza dhidi ya timu ya vijana wasiozidi umri wa miaka 18 ya Aston Villa katika ushindi wa 4-1. Kisha alifunga mabao tatu dhidi ya timu ya vijana wasiozidi umri wa miaka 18 ya Watford, na kuisaidia timu yake kushinda taji la Academy la Kundi A .

Mnamo Februari 2008, alicheza mechi yake ya kwanza ya timu hifadhi ya Arsenal dhidi ya Reading na alifunga bao la kipekee la Arsenal la mechi ingawa walipoteza mechi hiyo baada ya bao la Simon Church. Aliicheza timu ya vijana wasiozidi umri wa miaka 16 ya Arsenal katika ushindi wa Kombe la Atalanta, na alitajwa kama mchezaji bora katika shindano hilo. Alikuwa sehemu muhimu katika ushindi wa Arsenal wa kombe la vijana la FA mwaka wa 2009, kwani alifunga mabao katika nusu fainali na alitajwa kama mchezaji bora wa mechi baada ya kuonyesha mchezo uliosisimua katika mechi ya kwanza ya fainali dhidi ya Liverpool kwa kuandaa pasi mbili muruwa zilizosababisha mabao na kufunga bao moja mwenyewe.

Mnamo Julai 2008, Wilshere alichaguliwa katika timu ya kwanza ya Arsenal katika mechi za kirafiki ambazo zinachezwa kabla ya msimu kuanza. Alicheza mechi yake ya kwanza ya timu kuu dhidi ya timu ya kwanza ya Barnet kama mbadala wa Henri Lansbury baada ya nusu ya kwanza ya mechi na kuandaa bao lililofungwa nanJay Simpson. Wilshere alifunga mabao yake ya kwanza mawili ya Arsenal katika ushindi wa 10-2 dhidi ya Burgenland XI, na tena baadaye siku mbili katika mechi ya kirafiki dhidi ya Stuttgart.

Wilshere joto up kabla ya mchezo dhidi ya West Bromwich Albion

Meneja wa Arsenal Arsène Wenger alimpa Wilshere nafasi katika kikosi cha timu ya kwanza ya Arsenal msimu wa 2008-09, na alipewa jesi lenye namba 19. Alicheza mechi yake ya kwanza ya ushindani katika mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Blackburn Rovers kaatika uga wa Ewood Park mnamo Septemba 2008, kama mbadala wa Robin van Persie katika dakika ya 84. Akiwa na umri wa miaka 16 na siku 256, alikuwa mchezaji mchanga zaidi wa Arsenal milele kucheza mechi ya ligi kuu ya Uingereza, rekodi ambayo awali ilishikiliwa na Cesc Fabregas. Siku kumi baadaye, mnamo 23 Septemba, Wilshere alifunga bao lake la kwanza la timu kuu ya Arsenal katika ushindi wa 6-0 dhidi ya Sheffield United katika kombe la Carling.

Wilshere katika msimu wa mafunzo ya awali

Tarehe 25 Novemba 2008, Wilshere aliingia kama mbadala katika mechi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Dynamo Kyiv na kuwa mchezaji wa tano mwenye umri wa miaka kumi na sita milele kucheza katika Ligi ya Mabingwa barani. Mnamo Januari 2009 Wilshere alisaini mkataba wake wa kwanza wa utaalamu na kuiendeleza hadi Julai mwaka huohuo.

Katika maandalizi ya msimu wa 2009-10, Wilshere alifunga mara mbili na mara mbili alitajwa kama mchezaji bora wa mechi huku Arsenal ikishinda shindano hilo la kirafiki linalojulikana kama kombe la Emirates.

Tarehe 22 Septemba 2009, Wilshere alianza mechi ya Arsenal katika ushindi wa 2-0 katika Kombe la Carling dhidi ya FC West Bromwich Albion. Katika dakika ya 37 ya mechi hiyo, alihusika katika tukio la utata na Jerome Thomas kwani Thomas aliusukuma uso wa Wilshere na kumsababisha kuonyeshwa kadi nyekundu. Baada ya tukio hilo, meneja wa West Brom, Roberto Di Matteo, alisema kuwa Wilshere alimtusi Thomas na alijishinikiza baada ya kusukumwa.[1]

Wasifu wa Kimataifa

[hariri | hariri chanzo]

Tangu mwaka wa 2006, timu ya kandanda ya kitaifa ya Uingereza imeamua kumcheza Jack katika kundi la umri zaidi ya umri wake. Alipokuwa na umri wa miaka 15, aliichezea timu ya kandanda ya kitaifa ya Uingereza ya vijana wasiozidi umri wa miaka 17. Wilshere pia alikuwa na umri wa miaka 14 wakati aliichezea timu ya kandanda ya kitaifa ya Uingereza ya vijana wasiozidi umri wa miaka 16 mwaka wa 2006. Kisha alitajwa katika kikosi cha Uingereza ambacho kilishiriki katika shindano la kandanda la UEFA la vijana wasiozidi umri wa miaka 17 mwaka wa 2009 mwezi wa Mei, alianza mechi mbili za kwanza, hasa alisisimua katika mechi ya pili dhidi ya Ujerumani 2 kabla ya kuondolewa na jeraha ambayo ilimfanya asicheze mechi ya mwisho.

Pia amepokea sifa kutoka kwa meneja wa Uingereza, Fabio Capello ambaye alieleza kuwa kuna uwezekano kuwa kijana huyu wa Arsenal angejumuishwa katika kikosi cha Kombe la Dunia la mwaka wa 2010. Pia aliingia kama mbadala katika mechi yake ya kwanza ya timu ya Uingereza ya vijana wasiozidi umri wa miaka 21 dhidi ya Uholanzi.

Maisha ya Kibinafsi.

[hariri | hariri chanzo]

Jack alizaliwa katika {sehemu ya Stevenage, Hertfordshire na sasa katika sehemu ya Hitchin, Hertfordshire pamoja na wazazi wake. Alilelewa katika sehemu hiyo ya Hitchin na alihudhuria Shule ya msingi ya Whitehill na The Priory School. Alikuwa nahodha wa timu ya kandanda ya mwaka wa 9 ya The Priory School katika kombe la County, Kombe la Wilaya na nusu fainali ya Kombe la Kitaifa na alifunga mabao 38 njiani.

Takwimu ya Wasifu

[hariri | hariri chanzo]
(sahihi tangu 5 Desemba 2009)
Klabu Msimu Ligi! Kombe la FA Kombe cha Carling Ulaya Jumla
Matokeo Mabao Usaidizi Matokeo Mabao Usaidizi Matokeo Mabao Usaidizi Matokeo Mabao Usaidizi Matokeo Mabao Usaidizi
Arsenal 2008-09 1 0 0 2 0 0 3 1 1 2 0 0 8 1 1
2009-10 1 0 0 0 0 0 2 0 0 3 0 0 6 0 0
Jumla wa wasifu 2 0 0 2 0 0 5 1 1 5 0 0 14 1 1
  • Kombe la vijana la FA: 2009
  • FA Premier League Academy: 2009

Kimataifa

[hariri | hariri chanzo]
  • Victory Shield: 2006
  • Victory Shield: 2007

Kibinafsi

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Wilshere criticised over conduct". BBC News. 2009-09-23. Iliwekwa mnamo 2009-12-01.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]